Kwa mujibu wa ripoti ya mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Abbas Kaabi, Naibu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qum, katika hafla ya uzinduzi wa kitabu (Islam Eqameh)” iliyofanyika katika Kituo cha Tafiti za Kimkakati cha Hawza na Mapinduzi ya Kiislamu mjini Qum, huku akisisitiza uwezo wa Uislamu halisi wa Muhammadi (saww) wa kujenga ustaarabu, alitaja chanzo kikuu cha uadui wa Marekani, utawala wa Kizayuni na Magharibi kuwa ni “hofu ya kusimamishwa kwa dini na kutimia kwa Uislamu katika uwanja wa utawala na jamii.”
Akiwakumbuka kwa heshima na taadhima mashahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Vita vya Kujilinda Kitakatifu, mashahidi wa walinzi wa Haram, mashahidi wa usalama, afya, huduma, muqawama na mamlaka ya Iran — hasa mashahidi wakubwa kama Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah, Shahidi Sayyid Hashim Safi al-Din na makamanda mashahidi wa safu ya muqawama— alisema: Mashahidi hawa ni matunda ya kusimamishwa kwa Uislamu na ni alama ya jihadi katika njia ya kutimiza utawala wa Mwenyezi Mungu.
Naibu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walimu pia alimshukuru mwandishi wa kitabu “Islam Iqameh” na wahusika wa Kituo cha Tafiti za Kimkakati cha Hawza na Mapinduzi ya Kiislamu, hususan Hujjatul-Islam wal-Muslimin Mohseni, kwa juhudi zao za kielimu na upangaji wa mkusanyiko huu, na akakitaja kituo hiki kuwa ni miongoni mwa baraka za Mapinduzi ya Kiislamu.
Hofu ya Magharibi dhidi ya kusimamishwa Dini
Ayatollah Kaabi, huku akirejelea Aya Tukufu: «كَبُرَ عَلَى الْمُشْرِكِينَ مَا تَدْعُوهُمْ إِلَيْهِ», alisisitiza kuwa: Maadui wa Uislamu hawaiogopi Iran ya nyuklia au Iran yenye elimu na teknolojia pekee; kinachowatia hofu ni “kusimamishwa kwa Uislamu halisi wa Muhammadi na mafundisho ya Ahlul-Bayt (as)”. Magharibi haina tatizo na Iran iliyo imara lakini tegemezi na iliyodhalili; bali inaogopa Iran iliyo huru, yenye kutoa msukumo na inayojenga ustaarabu.
Aliongeza kuwa: Maadui wa Mapinduzi ya Kiislamu, baada ya kushindwa kwa miradi kama ISIS na mikondo ya kitakfiri, wameelekea kwenye miradi mipya; ikiwemo kuunda “Uislamu wa kiliberali,” “Shia wa kiliberali” na “Uislamu wa Kimarekani” kwa kuanzisha vyuo vikuu, taasisi za fikra na mitandao ndani ya ulimwengu wa Kiislamu. Lengo lao ni kuupokonya Uislamu maudhui yake ya mapinduzi na ya kujenga ustaarabu.
Ghaza; maonyesho ya aibu ya ustaarabu wa Magharibi
Ayatollah Kaabi, akirejelea uhalifu unaofanywa na utawala wa Kizayuni huko Ghaza, alisema: Kinachotokea Ghaza leo ni zao la elimu isiyo na imani. Ustaarabu unaotenganisha elimu na imani hufikia uhalifu mbaya zaidi kuliko wa Wamongolia na Unazi. Ghaza inapaswa kuchunguzwa na kuelezwa kama maonyesho ya fedheha ya ustaarabu wa Magharibi.
Aliendelea kusema: Uislamu unaosimamishwa ni mtindo unaounganisha elimu na imani, busara na maanawi, uadilifu na maendeleo, pamoja na mamlaka na rehema ya Mwenyezi Mungu. Akaongeza kuwa: Kwa mujibu wa kauli ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, Uislamu wa kiwango cha chini hautoshi; Uislamu lazima utekelezwe katika mifumo yote ya kitamaduni, kijamii, kisiasa, kiuchumi na ya utawala.
Maoni yako